Saturday, August 5, 2017

New Music: Cassie Signs to Bad Boy Ent/EPIC Records and Releases Single, “Love a Loser”



All those years on her back and knees finally paid off for one-hit-wonder Cassie Ventura. The 30-year-old model, who is best known as Sean Combs‘ concubine, signed a record deal with his label.

According to a press release, Cassie has officially signed to the roster of the Bad Boy Entertainment/Epic Records partnership.
After achieving platinum success with her debut single “Me & U” in 2006, Cassie returns with her first single in 4 years, “Love a Loser” featuring rapper G-Eazy.


“Love a Loser” is produced by Ben Billions & DannyBoy who crafted hits for superstars like Beyonce, The Weeknd and Young Thug.

Diva ajitosa ugumvi wa Madaha, Vanessa Mdee


KIMENUKA!Hii ndio kauli ambayo unaweza kuitumia baada ya Mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho Diva  kuingilia ugomvi unaoendelea kati ya Vanessa Mdee  na Baby Madaha.
Kwa muda mrefu Baby amekuwa akimponda Vanessa kuwa amekuwa akibebwa tu na hana uwezo wowote wa kuimba muziki wa kizazi kipya.
Kauli ambayo Diva ameipinga vikali na kumwambia Baby kuwa hana uwezo wa kujifananisha na Vanessa Mdee.
“Baby Madaha si wa kujifananisha na na Vanessa Mdee, ni vema akatafuta msanii wa kujifananisha naye .Anamzungumzia hivyo Vanessa yeye katoa nyimbo gani ambayo  watu wanaijua,”anasema.

Shilole amtetea mchumba wake

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shilole ameamua kila aina ya maneno kumtetea mchumba wake.
Mwanadada huyo anasema mchumba wake umri wake ni mkubwa na anajitambua na ndio maana amefika mahali amekubali kuwa atolewa na huyo mwanaume maana ni mtu mwenye umri mkubwa na anajiheshimu.
Anafafanua kuwa mwanaume wake wa sasa si kijana , ni mtu mzima na huwa hapendi mambo ya  mitandao na ndio maana hamuweki wazi.

Nawal aachika kwa Nuh Mziwanda

TAARIFA iliyopo kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile inayohusu madai ya kuvunjika kwa ndoa ya msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda na  mkewe Nawal .
Ndoa hiyo ilifungwa mwaka jana lakini inaelezwa imevunjika na sasa kila mtu anaendelea na maisha yake kivyake.
Akizungumza wiki hii Nawal anathibitisha kuachana na  baba mtoto wake Anyagile  na kila mtu anaishi maisha yake .
“Kwa sasa sina  mume wakati Nuh anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukristo) hakunishirikisha  kwa chochote .Hivyo nimerudi kwa bibi yangu na pia nimeshaolewa na mwanaume mwingine,”anasema.

Jini Kabula amtoa machozi Jackline Wolper

HALI ya mwigizaji Miriam Jolwa a.k.a Jini Kabula imewagusa wengi kwani kwa sasa anaonekana kama vime amechanganyikiwa kiasi cha kufanya mambo ambayo kwa akili ya kawaida ni ngumu kuyafanya.
Miongoni mwa wanaosikitishwa na hali ya staa wa Bongo Muvi Jacqueline Wolper ambaye ameoneshwa kuguswa na hali aliyonayo Jini Kabula kiasi cha kubaki akijiuliza maswali mengi bila majibu.
Kupitia kupitia kwenye Instgram yake Jacqueline anasema anatamani azungumze na Jini Kabula mambo mengi na anatamani  kumsaidia urudishe akili yake lakini swali ni kwamba amechelewa?
“Wasanii wenzangu tunamsaidiaje mwenzetu?Nini kimekuta.Hali aliyonayo Jini Kabula inaniliza sana,”anasema.
Jacqueline  anasema alikutana na Jini Kabula  akamwambia “We ni nimwanamke mzuri sana kwenye Bongo Muvi lakini natamani kujua tatizo nini .Hakunijibu akacheka tu  kisha akachukua nguo akaondoka sikupata muda wakuzungunza nae,”anasema.

Young Dee afafanua kuwa mbali na mtoto wake

MSANII wa muziki wa Hip hop, Young Dee ametoa ufafanuzi unaosababisha awe mbali ya mtoto wake kuwa inatokana na kubanwa na shughuli nyingi za kimuziki.
Ametoa ufafanuzi huo baada ya kuwapo kwa madai kuwa msanii huyo yupo mbali na mtoto wake na mama yake , hivyo anaeleza kuwa mbali ya mtoto na mama ni majukumu ya muziki na si kama ambavyo baadhi ya vyombo vinaripoti.

Witness ageuza ubonge wake kuwa fursa

MWANADADA mwenye umaarufu wake kwenye muziki wa kizazi kipya na hasa kutokana staili yake  akiwa na kundi la Wakilisha Witness amasema hatasahau kipindi kigumu alichopitia baada ya mimba yake kuharibika.
Akielezea zaidi aina ya maisha aliyopitia kipindi hicho,Witnes anaeleza baada ya ujauzito wake kuharibika, alijihisi kama ametengwa na kuwa mpweke , hali iliyomfanya we anakula hovyo na matokeo yake mwili wake ukawa kibonge.
Baada ya unene kuzidi akaiona hiyo ni fursa na akaamua kutumia mwili wake kama fursa na alianza kujifunza kuhusu dawa za kupunguza uzito na kuufanya mwili kuwa mwepesi, biashara anayoifanya hadi hivi sasa na imesaidia wengi.

Ukubwa wa matiti wamkera Amber Rose

STAA wa Marekani, Amber Rose ameonesha kukerwa na ukubwa wa matiti yake ambapo imefika hatua anashindwa kuvaa blauzi ndogo.
Amber Rose ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa 21 Savage, anasema ukubwa matiti yake sasa unamfanya afikirie hata kufanya upasuaji kupunguza matiti yake.
Kupitia mtandao wa Instagram Amber amebainisha hayo “Nafikiria kufanya upasuaji ili kupunguza ukubwa wa haya matiti yangu ambayo yananinyima  raha na nashindwa hata kuvaa blauzi ndogo.”

Ukaribu wa 50 Cent, Jasmin wauibua maswali

UKARIBU uliopo kati ya mkongwe wa muziki wa Marekani  50 Cent na mwanadada muigizaji wa vichekesho Jasmin Brown umeibua maswali mengi kwa mashabiki wake.
Wawili hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara wakiponda raha kwenye maeneo tofauti na hiyo imefanya watu kuhisi huenda wana mahusiano wa kimapenzi.
Hata hivyo Jasmin amekuwa akiposti picha inayowaonyesha wakiwa pamoja na kueleza kwenye mtandao wake kuwa anajisikia vizuri kufanya kazi kila siku na bosi wake mpya.
Tayari  50 Cent amekanusha taarifa hizo na kueleza kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yoyote.

Rihanna awakumbuka wasichana Malawi

MWANAMUZIKI  Rihanna ameamua kutoa msaada wa baiskeli kwa wasichana nchini Malawi kwa lengo kuwasaidia kwenda shuleni  kupata elimu.
Rihanna anasema msaada huo unatokana na mojawapo ya ushirikiano kati ya Wakfu wa mwanamuziki huyo wa Clara Lionel Fountaion na kampuni moja ya baiskli kutoka China Ofo.
Hivyo kupitia kampeni ya 1km Action itatoa ufadhili huo ili mamia ya wasichana wahudhurie shule za upili nchini malawi.
Na wale watakaofuzu kupata ufadhili huo watapewa baiskeli ili kuhakikisha wanakwenda shule.Kulinga na wakfu huo kuna takriban wanafunzi milioni 4.6 nchini Malawi lakini ni asilimia nane pekee wanaokamilisha masomo yao ya shule za upili.

Celebrity Style: Beyonce Knowles Wearing Louis Vuitton x Supreme

A post shared by Industry On Blast (@theindustryonblastx) on

Daycare singer Beyonce emerged from her twins’ nursery to go out on a romantic dinner date with her husband, rapper Jay-Z, on Thursday.

Sharp-eyed fans noted the 37-year-old mother-of-3 carrying a red epi leather Louis Vuitton x Supreme clutch, which retails for $1,100.
Other sharp-eyed fans noted Beyonce still hasn’t dropped her baby weight after reportedly giving birth to twins in June.
The Louis Vuitton x Supreme limed edition collection caused a frenzy at a pop up store in Miami in June. Louis Vuitton cancelled the remaining pop up store locations in Dallas and New York City after reports that people were camping out on the sidewalk outside the stores.
The fashion house decided to sell the coveted items to their VIP clients such as Beyonce and other wealthy socialites and ballers.
You can still find Louis Vuitton x Supreme items on eBay and Craigslist at a very high markup.



Louis Vuitton x Supreme
Louis Vuitton x Supreme

This is an open post where you can discuss any subject matter. This post will not be censored or moderated. Disqus may automatically moderate certain words considered offensive. There are no rules in Open Posts. So enter at your own risk.

Harmonize amkingia kifua Zari


MSANII kutoka Lebo ya WCB Harmonize amemtetea Zarina Hassan ‘The Boss Lady ambaye alikwenda Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kula bata ikiwa ni siku chache zimepita tangu  afiwe na mama yake mzazi.
Zari baada ya kupatwa na msiba huo baba wa watoto wake Diamond aliamua kumpeleka Mombasa kwa ajili ya kumliwaza lakini baada ya tukio hilo baadhi ya watu wakaanza kumponda Zar wakidai hana uchungu na mama yake.
Hivyo,Harmonize anasema mtu akipata matatizo halafu akaenda sehemu nzuri ili kujifariji si jambo baya”Sote tunafahamu kufiwa kunaumiza na si kitu cha kusahau kirahisi ,”anasema.
Anasema kifo ni kitu cha lazima kwa kila binadamu na kinapotokea kwa mmoja wetu lazima uumie lakini maisha mengine lazima yaendelee kwani hata ukikaa ndani miaka saba haitasaidia na aliyekufa hatarudi.”Hivyo Zari kwenda kwenye mazingira ya kumpa faraja si vibaya”.

Shetta haamini katika nyimbo nyingi

MSANII wa Bongo Fleva Shetta amesema kuwa wimbo wake mpya wa Wale Wale ni jibu kwa mashabiki waliokuwa wanataka asikae muda mrefu bila kutoa nyimbo.
Akizungumza kuhusu ujio wa wimbo huo mpya anasema anaamini kwenye  kazi anayoifanya na yupo mbioni kutoa nyimbo nyingine mpya kati moja au mbili.
“Hakuna sababu ya kufanya vitu ambavyo watu wanasema au wanafikiri ni sawa.Natakiwa niamini katika kitu ambacho nafanya,”anasema Snhetta.
Pia anasema kwa kuwa mashabiki wake anataka wabadilike atafuata wanachopenda lakini kwenye moyo wake haamini katika kutoa nyimbo nyingi.

Mwana FA apania video zenye ubora

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva  Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA amesema moja ya mikakati yake ni kuendelea kufanya video kali.
Mwana FA anafafanua baada ya kuanza kufululiza kufanya video za muziki wake nje ya Tanzania ameona mabadiliko ya muziki wake hasa hasa katika upande wa video na hivyo jukumu lake ni kuendelea kutoa video bora.
“Nataka hata nikienda nchini Marekani nikionyesha video zangu waseme safi.Lazima niendelee kuthibitisha uwezo wangu kwenye game,”anasema.

Ada Slim, Tonto Dikeh wazua gumzo

MTAYARISHAJI wa filamu za Nigeria, Ada Slim amedai alikuwa akimpa rushwa msanii mwenzake, Tonto Dikeh na si kweli ndiye aliyesababisha kupata umaarufu.
Tonto alijibu kwa kusema hakuwa kufanya hivyo na pia hakuwahi kuomba fedha yoyote kwake.
Ada Slim alisema hazungumzi hayo kwakuwa aliwahi kumuazima fedha au gari lake lakini ni kutokana na kumcheka wakati baba yake alipofariki.
Licha ya kwamba katika ukurasa wake wa Instagram hakutaja jina la aliyemtuhumu, lakini alindika:” Huna sababu ya kunicheka, sote tutawazika wazazi wetu, sitomuombea yeyote aondokewe na mzazi wake. kila la kheri dada.

Oshodi-Oke hataki kuwasikia waandishi

MSANII mkongwe wa filamu za Nollywood,  Ronke Oshodi-Oke amesema hapendi kuhojiwa kwakuwa hutafsiriwa na kukaririwa vibaya ndio maana hataki kufanya hivyo.
Ronke ambaye alikuwa akiwasiliana vizuri na televisheni moja, alilamika kwamba mahojiano mengi hayawekwi kama alivyohojiwa.
Alisema mahojiano mengi yanayofanywa huwa hayawekwi kama inavyotakiwa ila huchaguliwa maeneo yanayoonekana kwao ni kuzuri zaidi.
“Ndio mana sifanyiwi sana mahojiano kutokana na hali kama hivyo, waandishi wanaweka habari wanayotaka wao bila kujali muhusika unaichukuliaje,”.

Msanii aliyedaiwa kufa avunja ukimya

MSANII mkongwe wa filamu za mapigano za Nigeria ‘Yoruba’, Iyako Oko amesema bado yupo hai na kwamba anaendelea na matibabu nchini India.
Kauli hiyo imekuja baada ya ukimya wake wa muda mrefu uliotokana na kudaiwa alipooza mwili kulikosababisha kufariki dunia.
Lakini akizungumza na mtandao wa Gbolahan Adetayo, mwanamama Iyako alisema kwa sasa anapambana na tatizo na upungufu wa damu unaonekana alirithi katika familia yao.
“Tatizo lilianza siku moja wakati naamka nikajikuta siwezi kutembea na kuhisi sehemu ya mwili umepooza, nilichukuliwa na kupelekwa hospitali na kutibiwa lakini ikaonekana hali si nzuri wakati huo nikitibiwa Hospitali ya Jeshi iliyoitwa 68 mjini Yaba, Lagos”,
“Walijitahii kadri walivyoweza lakini sikuweza kuzungumza kwa mwezi mmoja, namshukury Mungu muweza wa yote nikapata nafuu, sikupooza mguu na mkono ulifanya kazi kama kawaida’
Aliongeza kwa sasa anaendelea vizuri na ana ratiba ya kwenda hospitali kuangalia maendelea mara kwa mara.

Segun atamani kuimba na Tekno

MWANAMUZIKI ambaye pia ni msanii wa Nollywood, Segun Arinze amewashangaza wengi baada ya kusema angependa kufanya wimbo na msanii Augustine Miles Kelechi ‘Tekno’.
Kwa sasa nimeelekeza nguvu katika kipaji changu cha uigizaji na Utangazaji, kama unavyojua nafanya kipindi cha ‘Give and Take Lottery’ katika televisheni.
Ndipo alipoelekeza nguvu lakini pia anataka kufanya kolabo hasa na msanii Tekno na kwamba anampenda na ni shabiki wake mkubwa.
Ingawaje anawapenda pia Davido, Wizkid, Tekno, Phyno na waliobaki; “Ninapenda kwa jinsi anavyofanya kazi zake.
Alisema kwa wakati ujao anaweza kufanya hivyo na itakuwa kolabo kati ya kijana na mzee kitu ambacho kitakuwa cha kipekee.
Mbali na msanii huyo, pia alisema anaweza kufanya nyimbo na wasanii kama Timi Dakolo, Wizkid, Davido lakini hakupenda kuzungumzia kwa kina.