MSANII mkongwe wa filamu za mapigano za Nigeria ‘Yoruba’, Iyako Oko amesema bado yupo hai na kwamba anaendelea na matibabu nchini India.
Kauli hiyo imekuja baada ya ukimya wake wa muda mrefu uliotokana na kudaiwa alipooza mwili kulikosababisha kufariki dunia.
Lakini akizungumza na mtandao wa Gbolahan Adetayo, mwanamama Iyako alisema kwa sasa anapambana na tatizo na upungufu wa damu unaonekana alirithi katika familia yao.
“Tatizo lilianza siku moja wakati naamka nikajikuta siwezi kutembea na kuhisi sehemu ya mwili umepooza, nilichukuliwa na kupelekwa hospitali na kutibiwa lakini ikaonekana hali si nzuri wakati huo nikitibiwa Hospitali ya Jeshi iliyoitwa 68 mjini Yaba, Lagos”,
“Walijitahii kadri walivyoweza lakini sikuweza kuzungumza kwa mwezi mmoja, namshukury Mungu muweza wa yote nikapata nafuu, sikupooza mguu na mkono ulifanya kazi kama kawaida’
Aliongeza kwa sasa anaendelea vizuri na ana ratiba ya kwenda hospitali kuangalia maendelea mara kwa mara.

0 Comments:
Post a Comment