Saturday, August 5, 2017

Diva ajitosa ugumvi wa Madaha, Vanessa Mdee


KIMENUKA!Hii ndio kauli ambayo unaweza kuitumia baada ya Mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho Diva  kuingilia ugomvi unaoendelea kati ya Vanessa Mdee  na Baby Madaha.
Kwa muda mrefu Baby amekuwa akimponda Vanessa kuwa amekuwa akibebwa tu na hana uwezo wowote wa kuimba muziki wa kizazi kipya.
Kauli ambayo Diva ameipinga vikali na kumwambia Baby kuwa hana uwezo wa kujifananisha na Vanessa Mdee.
“Baby Madaha si wa kujifananisha na na Vanessa Mdee, ni vema akatafuta msanii wa kujifananisha naye .Anamzungumzia hivyo Vanessa yeye katoa nyimbo gani ambayo  watu wanaijua,”anasema.

0 Comments: