Saturday, August 5, 2017

Nawal aachika kwa Nuh Mziwanda

TAARIFA iliyopo kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile inayohusu madai ya kuvunjika kwa ndoa ya msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda na  mkewe Nawal .
Ndoa hiyo ilifungwa mwaka jana lakini inaelezwa imevunjika na sasa kila mtu anaendelea na maisha yake kivyake.
Akizungumza wiki hii Nawal anathibitisha kuachana na  baba mtoto wake Anyagile  na kila mtu anaishi maisha yake .
“Kwa sasa sina  mume wakati Nuh anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukristo) hakunishirikisha  kwa chochote .Hivyo nimerudi kwa bibi yangu na pia nimeshaolewa na mwanaume mwingine,”anasema.

0 Comments: