MALKIA wa filamu za kibongo, Wema Abraham Sepetu ameweka wazi bado hajaona mtu wa kumshusha katika maisha yake na kama yupo basi bado hajazaliwa.
Sepetu aligamba kwamba kwani yeye alivyo ni majaaliwa kutoka kwa maulana na si kujitakia.
Mlimbwende huyo ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuna mtu kamharibia siku na kumwambia yeye hakujitakia kuwa alivyo hivyo mtu huyo ajue kutofautisha.
“Wa kunizima hajazaliwa bado jamani...halafu mjue kutofautisha kati ya kujaaliwa na kujitakia...alhamdulillah nyingi kwa maulana wangu... sikujitakia...ni majaaliwa tu...kuna mtu kajua kuniharibia siku wallah,” aliandika Wema Sepetu katika mtandao huo.
Aidha Wema aliongeza kwa kusema katu hawezi kujitutumua kwani anaogopa kujiumiza.
Vilevile tukio hilo linaunganishwa moja kwa moja na mtu ambaye Wema amemhisi anataka kujaribu kudukua mtandao wake wa Instagram hali iliyosababisha kumuandikia ujumbe kuwa katu hatamweza hivyo awe mpole.

0 Comments:
Post a Comment