Saturday, September 9, 2017

Lil Wayne kukaa benchi wiki mbili

RAPA wa kimataifa, Lil Wayne Jumapili ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya hali yake kuendelea vizuri ikiwa ni siku chache baada ya kupata kifafa akiwa hotelini na kujikuta hajitambui.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeripoti kuwa Wayne ameruhusiwa kutoka hospitali aliyokuwa amelazwa mjini Las Vegas.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na madaktari, rapahuyo anatakiwa kupumzika kwa kipindi cha wiki mbili bila kufanya kazi yoyote ikiwemo kupanda jukwaani kutumbuiza.
Kwa hiyo Lil Wayne atatarajiwa kuonekana tena jukwaani kwenye tamasha lake la Septemba 23, mwaka huu.

0 Comments: