Saturday, September 2, 2017

Picha za utupu zamponza Amber Lulu

MUUZA sura maarufu katika video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva Amber Lulu amejikuta akifikishwa Kituo cha Polisi Urafiki jijini Dar es Salaam ili kutoa maelezo baada ya kusambaa mitandaoni kwa picha alizopiga akiwa utupu pamoja na mwanamuziki mwenzie, Young D.
Amber Lulu alifikishwa kituo hicho cha polisi wiki hii na kuachiwa saa chache baadae baada ya kukamilisha kutoa maelezo aliyotakiwa.
Inaelezwa sababu za kuhojiwa huko kulitokana na kusambaa kwa picha hizo mtaoni ambazo kimsingi hazikuwa na maadili ya Kitanzania.Picha hizo zinamuonesha Amber Lulu akiwa ameficha matiti yake kwa mikono huku akiwa amevaa nguo ya ndani inayomuonesha mwili wake.Wengi wamekerwa na picha hizo

0 Comments: