Saturday, September 2, 2017

Malaika akana kufanana na Lulu Diva


MREMBO anayetesa kwenye muziki wa kizazi kipya Malaika amesema yeye hawezi kujifananisha na Lulu Diva kwasababu kila mmoja anafanya aina yake ya muziki.
Akizungumzia hilo, anasema kuwa anatambua Lulu Diva ni msanii mpya na anayefanya vizuri kwenye muziki na wanaowalinganisha hawafanyi kitu kibaya.
Anafafanua kwake hawezi hawezi kujilinganisha ila watu wanaowafuatilia ndio wanaweza kuwalinganisha”Niseme tu Malaika ni Malaika. Ukinisikiliza vizuri katika miziki yangu na namna ninavyotunga.”
“Nikiri sijafanikiwa kusikiliza miziki yake lakini najua ule mmoja ëUsimuacheí, kwa hiyo najua yupo tofauti na mimi.Najua kuna vitu anapenda kutoka kwangu. Inatokea mtu anakupenda kiasi cha kutamni kufanya kama ambavyo unafanya na ndicho ambacho huenda kimetokea”.

0 Comments: