Saturday, September 9, 2017

Tunda afunguka, asema picha za utupu hazina dili


VIDEO Queen, Tunda Sebastian amewapa makavu mamodo wanaoibuka kwa staili ya kupiga picha za utupu akisema fasheni hiyo hivi sasa imefeli, hivyo ni bora wakatafuta namna nyingine ya kutoka.
Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema wasichana wanaokuja na kudhani kuwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni kutawafanya wawe maarufu wamechemsha kwa sababu wanachofanya ni ujinga uliopitiliza.
“Ninachokiona hapo ni upumbavu tu na tamaa ya umaarufu bila kutafakari madhara yake, kifupi watafute plan B maana A imefeli na kuwadhalilisha,” alisema.

0 Comments: