MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Saleh ‘Alikiba’ ambaye anafanya vizuri na kibao cha Seduce Me, amejigamba kuwa kuimba muziki mzuri kunamfanya akubalike na jamii yake.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, alionesha kufurishwa na mapokezi ya kazi zake katika jamii na anajivunia muziki mzuri anaofanya huku akitumia nafasi hiyo kuwaambia kuwa wategemee kupata mambo mazuri zaidi.
“Muziki mzuri ukitoa kila mtu anaukubali haijalishi kwamba huyo ni kiongozi au mheshimiwa watu wanasikiliza muziki kwa sababu ni sehemu ya maisha yao,” alisema.
“Nimefurahi sana kwa kweli namna muziki umetanuka na kufika mbali. Inaniongezea nguvu ya kufanya kazi nzuri ambayo nahisi itaizidi kuipeleka Tanzania yetu mbele kutangaza lugha ya Kiswahili,”.
Ngoma ya Seduce Me ilitoka Agosti 25, mwaka huu na hadi sasa ina viewers milioni 4.6 katika mtandao wa YouTube.

0 Comments:
Post a Comment