NYOTA wa filamu za Nollywood, Tonto Dikeh ambaye ndoa yake ipo chini ya mwaka, ilipata misukosuko lakini sasa amejipanga kuanza upya maisha ya ndoa.
Mwanadada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alifanyiwa mahojiano hivi karibuni na kusema;” Nimekuwa nje ya uigizaji kwa muda mrefu ila nimerudi kwa kishindo. Nitaanza kwa kuachia filamu yangu ‘Celebrity Marriage’ hivi karibuni.
Alisema amekuwa mpya kwakuwa amerudi tena katika uigizaji na hataki kujihusisha na masuala kama ambayo yalitokea awali.
Aliongeza hatoi filamu hiyo kwakuwa anatafuta umaarufu ila ameamua kuingiza kitu kipya chenye ubora sokoni.
Alisema familia yake ilimshauri awe anatoa filamu tano kwa mwaka lakini ameamua awe anatoa tatu lakini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

0 Comments:
Post a Comment