Tuesday, August 15, 2017

Majid eti hataki ngono kabla hajaoa

MSANII wa Nollywood ambaye ni mzaliwa Ghana, Majid Michel amelaani vitendo vya ngono kabla ya ndoa kwani ni dhambi ya uasherati ambayo ni kinyume na maandiko ya Mungu.
“Falsafa yangu katika maisha ya ujana hairuhusu kujihusisha na ngono kwasababu ni kinyume na maandiko ya Mungu. Maneno kama haya yanapaswa kuzungumzwa kwa hisia kwani ngono ina nguvu katika maisha yetu endapo ukijiingiza,” alisema.
Katika mahojiano yake, Majid alisema;”Wanawake waliolewa ambao huwakana waume zao ndio wanaowasababishia waume zao kupata tiketi ya kuwadanganya”.
Alisema ni jukumu la mwanamke kujitoa kwa mmewe hata kama hawajisikii kufanya hivyo, endapo mwanaume atajengwa katika mazingira hayo ataweza kutatua matatizo yaliyopo.
Alipoulizwa endapo ataendelea kuigiza sehemu za mapenzi,alijibu” Mimi ni msanii nina thamani na maadili yangu, siwezi kucheza sehemu ambayo naona inaweza kuleta matatizo katika maisha yangu ya kila siku”

0 Comments: