Tuesday, August 29, 2017

Namba 23 yampa mafanikio DJ Khaled

ALBAMU ya Grateful ya DJ Khaled kwa sasa inaonekana kuwa moja ya albamu bora na kusababisha kuwe gumzo kwa mashabiki wa muziki wake.
Tangu alipoitoa albamu hiyo Juni 23 mwaka huu imekuwa ikifanya vema na inampa mafanikio makubwa.
Akizungumzia albamu hiyo anasema imepokelewa vema na mashabiki wa muziki huku akiamini namba 23 ikiwa ni ya bahati kwake na ndio yenye mafanikio makubwa.
Pia DJ Khaled kupitia akaunti yake ya Instagram anaelezea  umuhimu wa namba hiyo katika maisha yake huku ikimuhusiha kupata mtoto wake wa kwanza Oktaba 23 mwaka jana.

0 Comments: