SANAA imekuwa ajira muhimu ambayo imeyafanya maisha ya vijana wengi nchini kuimarika na kuongeza kipato chao bila kujali kiwango cha elimu ambacho wanacho,
Mafanikio ya sanaa yametawaliwa na kipaji, juhudi, nidhamu wala elimu haijawahi kuwa na nafasi kubwa mbele yake.
Napenda uthubutu ambao umekuwa ukifanywa na vijana katika kuwekeza akili, nguvu na fedha zao kuhakikisha wanatoboa kwenye tasnia hii iliyojizolea mashabiki lukuki nchini.
Ni wazi kuwa katika listi ya wasanii waliofanya makubwa kwenye nchi hii yapo majina ya watoto wa kike, yaani kwenye kila kundi la veterani watatu waliofanya vema jina la mrembo mmoja litachomoza, unabisha? Twende taratibu!
Tuanzie kwenye taarab, utakutana na Siti Binti Saad na rekodi zake tamu ikiwemo Yalaiti ambayo baadaye Bi Kidude aliirudia, hebu utazame mchango wa Mama mwenye sauti ya ëkasukuí kutoka Kilimanjaro Band, Patricia Hillary, ukiketi na Linah Sanga atakuambia huyo ndio aliyemvutia kuingia kwenye sanaa ‘Mentor’.
Yote tisa, 10 jina la Lady Jay Dee, dada wa nguvu ambaye hakuna asiyeujua mchango wake kwenye muziki wa Bongo Fleva aliwekeza kila kitu chake na leo hatuwezi kumsahau hata kama hayupo kwenye kilele chake ambacho kiliwafanya mashabiki wamuone Jennifer Lopez wa Bongo.
Muziki wetu umekuwa, wapo majemedari waliofanya makubwa na tunapaswa kuwapa heshima yao, wapo vijana waliokuja hivi sasa na ukweli wanatuonesha maana ya msemo wa ‘vijana ni nguvu kazi’ Diamond, Ali Kiba ni mifano halisi kwa jinsi walivyoubadilisha muziki kuwa wa kisasa zaidi.
Jambo ambalo linaumiza ni kuona yule aliyekuwa anatamba jana eti leo hii ameanguka na wala hasikiki tena na wale mashabiki waliokuwa wakituma ‘message’ kwenye Radio na TV kuomba nyimbo zake sasa hawatumi tena.
Eti yule aliyekuwa akijaza shoo na kutamba kwenye mitandao ya kijamii huku ukubwa wa jina lake ukizidi kupanda, ghafla bila sababu ya kueleweka ameanguka na hakuna mwenye habari nae, ndivyo Bongo Fleva ilivyo, ndivyo wasanii wetu walivyo watapanda leo, kesho watateleza ilihali ardhi ni kavu.
ANGUKO LA WASANII WA KIKE!
Kabla ya anguko la Jide kwenye muziki tayari anguko la Ray C mrembo ambaye alifanikiwa kuyateka yale magazeti ya udaku kabla hata ya Facebook kuingia mjini lilishatokea, na watu wakamleta Rachel kama mrithi wake lakini cha kusikitisha huyo mrithi nae kaanguka.
Aliingia kwa nguvu Mwasiti mmoja kati ya mabinti wanaoimba bila kubahatisha ingawa jina lake halijawahi kuandikwa na kusifiwa kwa namna ilivyomstahili, tulibaki kukiri Mwasiti anaimba! anaimba! anaimba sana!
Lakini kamwe heshima yake haijawahi kuwa ile yenye kumfanya ajivunie.
Tunavyozungumza hivi sasa amebaki na jina lake na wala hakuna ambaye anamkumbuka tena kwamba ni yeye aliyetesa na Hao, Nalivua pendo na nyingine kali
Na hata alivyorudi na Serebuka tayari walishaanza kumsahau.Nani ambaye aliuvamia huu muziki kwa namna yake zaidi ya Linah? Sauti nyororo, umbo lililoongeza thamani yake vikamfanya auteke muziki wetu akasumbua sana na ikaonekana katika listi ya wasanii ambao watatoboa kimataifa yeye ni mmoja wao, unajua ilikuaje?
Agosti 2015 aliachia kichupa chake cha Ole Themba alichokifanyia ‘Sauzi’ kwa God Father, bonge la wimbo, video yenye heshima ikatikisa kila kona na kila mmoja akaona mwanzo wa mafanikio makubwa ya Linah.
Haikua hivyo mambo yakavurugika na kila kitu kikapotea leo amebaki kuwa msanii wa kawaida hakuna anaekimbilia Radio yake akisikia Linah anafanya ‘Interview’, nuru iliyokuwepo mwanzo imeondoka! Hii ndio Bongo Fleva!
Inaumiza kuona wasanii wa kike wakishindwa kuonesha muendelezo mzuri wa kasi ambayo wamekuwa wakianza nayo, haieleweki kwanini wameshindwa kulinda majina yao, fikiria kasi aliyoingia nayo Ruby eti leo hayupo tena kileleni, nini kimetokea? Hatujui! na wala tusiongelee zile tetesi tunazosikia kuhusu yeye.
VANNESA AMEBEBA MATARAJIO YETU?
Nawaza tena kuhusu kuondoka kwa kasi kwenye muziki kwa wasanii wetu wa kike, tukubali tukatae bado hatujawaa na msanii wa kike ambaye anaweza kutupa kile alichotuonesha Jide, ingawa wapo na wanakuja wasanii wakali.
Najua unasubiri tumuongelee Vanessa, ndiyo nataka tumjadili pamoja hivi kuna mwanga wowote unaouona kwa Vee Pesa? Naomba hapa tusishikane mashati sijasema Vee hajui au ameanguka lakini tuulizane anaweza kuzuia anguko lake?
Muonekano wa kisanii, uwezo mkubwa anapokuwa kwenye ëboothí mnyama wa kumiliki steji, zaidi kinachomuweka juu ya wasanii wengine hata wale wa kiume ni ëconnectioní aliyonayo kimataifa.
Vanessa anajuana na wasanii wengi wa nje na uwezo wa kufanya nao collabo anao lakini naona kama amepoa sana, nimejiuliza au ni vile hana changamoto kutoka kwa wasanii wengine wa kike?
Tujiulize toka ametoka mbona hajabadilika kuwa wa ‘ajabu’ kama ilivyo kwa Diamond?
Kwa levo ambayo tulijiaminisha kwake tulitarajia leo hii awe anazurura nje ya nchi kufanya collabo na shoo za kutosha, ila haijawa hivyo tupo nae hapa, pamoja na ukubwa wa video na rekodi zake kutikisa katika Media zetu bado siyaoni mafanikio tuliyomtabiria kimataifa.
Inawezekana amekosa changamoto kutoka kwa wenzake kwa sababu kiuhalisia yule Yemi Alade wa Nigeria hakuna chochote anachomzidi Vee lakini tayari kashatangulia mbele na ni mmoja wa wasanii wakubwa Afrika.

0 Comments:
Post a Comment