Tuesday, August 22, 2017

Matapeli wamtumia Jenifa wa Kanumba kutapeli

MWIIGIZAJI wa filamu za kibongo ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia filamu za marehemu Kanumba, Hanifa Daudi amesema matapeli wanaotumia jina lake mtandaoni kufanya utapeli wanamuumiza kichwa.
Kwa mujibu wa Hanifa ni kwamba matapeli hao wamefungua akaunti ya feki ya jina lake kwenye mtandao wa Facebook na Instagram na kisha kuanza kuomba fedha kwa watu mbalimbali.
“Naumia sana jamani, hebu nisaidieni, sina akaunti kwenye Facebook, kwani ni juzi tu mama alinishauri nifungue akaunti ya Instagram ili kujitofautisha na hao matapeli.
“Sina simu na hiyo akaunti siitumii, kwa sasa nipo Tanga masomoni, wanatumia jina langu kutapeli.Eti wanajiita Hanifa Jennifer Kanumba na wanaposti picha zangu, sijui wanazitoa wapi,”anasema.

0 Comments: