Tuesday, August 15, 2017

Mama wa Wiz Khalifa amfungulia kesi mkwewe


MAMA mzazi wa mwanamuziki nyota, Marekani, Wiz Khalifa, ameamua kumfungulia kesi ya udhalilishaji aliyekuwa mkwe wake Amber Rose baada ya kumtolea kauli za kumtuhumu kuwa ni mama asiyefaa kulea mjukuu wake Sebastian.
Pia anadai Amber Rose amemuita kuwa ni mhalifu na kumhusisha na kifo cha bintiye ambaye ni dada wa Wiz Khalifa.
Hivyo kutokana na tuhuma hizo mama huyo ameamua afungue kesi dhidi ya mwanamitindo huyo.Katika kesi hiyo mama wa Wiz Khalifa anadai Sh milioni 100 kutoka kwa Amber Rose ambaye hadi sasa hajajibu loloteza zaidi ya kuwa kimya.
Pia hata kwenye mitandao yake ya kijamii Amber Rose amekuwa kimya kwa kutoandika chochote wakati mama huyo akiwa tayari amefungua kesi hiyo.
Kwa kukumbusha tu Wiz Khalifa na Amber Rose walifunga ndoa Julai mwaka 2013.Wakiwa kwenye ndoa walifanikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Sebastian.
Hata hivyo baada ya mama yake kumfungulie kesi mkwe wake mwanamuziki huyo hajazungumza chochote.

0 Comments: