Saturday, August 26, 2017

Chika Ike aanika maungo yake mtandaoni

MSANII wa Nollywood, Chika Ike amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kufanya tangazo la biashara akiwa nusu uchi.
Mwanadada huyo ambaye kwasasa yupo tayari na kuendelea na msimu wa tatu wa kipindi chake televisheni cha African Diva, tayari ameshaanza kuachia matangazo yake.
Chika ambaye alisherehekea kuachwa kwakwe mwaka uliopita, aliweka katika mtandao wake wa kijamii video ya tangazo alilofanya kwa ajili ya kipindi hicho.
Alionekana akiwa mwenye kushawishi huku akilala katika bafu maalumu lililotengenezwa na kuwaonesha mashabiki wake kilichomo ndani ya mwili wake.
Tangazo hilo lilikuwa na lengo kupromoti kipindi chake hicho ambacho tayari kimeshaangaliwa mara 28,000.

0 Comments: