Saturday, July 22, 2017

Wasanii Nollywood wagombea bwana

 Angela Okorie 
A post shared by Angela Okorie (@realangelaokorie) on

UHUSIANO wa nyota wa filamu za Nollywood, Angela Okorie na Anita Joseph, umeingia shubiri baada ya kudaiwa kugombea mwanaume.
Wawili hao ambao wana urafiki ulioshibana, hivi sasa kila mmoja amejiondoa urafiki kwa mwenzake katika mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu ya nyota hao, baada ya Anita kuona rafiki yake ameweka picha za mpenzi wake katika ukurasa wa Instagram ndipo ugomvi ulipoanza.
Wanadada hao walikuwa wakifanya kila kitu pamoja lakini tangu tukio hilo litokee kila mmoja anapita njia yake hasa baada ya kurushiana mvua ya matusi kwa maneno.
Inaelezwa kwa sasa hata kuonana hawataki.



 

0 Comments: