Saturday, July 22, 2017

Jay Mo afunguka ugumu wa muziki

MSANII wa Bongo Fleva Juma Mohamed maarufu Jay Mo amesema changamoto iliyopo kwa sasa katika muziki huo ni ugumu uliopo ikilinganishwa na zamani na ndio maana kuna wasanii wengi wenye uwezo mkubwa leo wako pembeni.
Jay Mo ambaye ambaye amejijenge jina kutokana na staili yake ya kuimba muziki huo anafafanua mazingira ya kujitengeneza ‘brand’ na kusukuma muziki ufike mbali ni changamoto kwa wasanii wakongwe kwani wengi hawakuzoea masuala ya mitandao au video zaidi ya kuandaa ngoma kali zenye ladha ya kipekee.
Hata hivyo anasema kuhusu muziki wa sasa hivi ukiufuatilia utabaini kuna wasanii wakali ila wanashindwa kuingia ndani yake kwasababu ya mazingira ya game yalivyo na kuongeza game inahitaji vitu vingi ambavyo kuvifanya mpaka uwe na fedha au uwe chini ya uongozi unaoweza kukugharamia.

0 Comments: