Saturday, July 22, 2017

Tonto Dikeh aolewa tena!

MWANADADA aliyejizolea umaarufu katika filamu za Nollywood, Tonto Dikeh ameolewa tena! Ndivyo anavyoonekana katika filamu mpya inayoandaliwa hivi sasa na msanii huyo.
Tonto ambaye aliachana na mumewe kutokana na kupigwa kila wakati, ameonekana ameibuka na ushindi katika filamu hiyo mpya.

Nyota huyo ni miongoni mwa mastaa wa Nollywood ambao kwa sasa wanandaa filamu za kuoana iliyo chini ya Uchenna Mbunabo mjini Lekki Lagos.
Katika filamu hiyo, Tonto anacheza kwa mwanamke aliyepitia wakati mgumu katika ndoa yake hadi kupigwa kitu ambacho kinaelezea uhalisia wa maisha yake.
Filamu hiyo inaonekana kama kutimiza ndoto za mwanadada huyo ambaye anataka kutumia usanii wake kufikisha ujumbe kwa jamii kutokana na yaliyomkuta.

A post shared by Tonto•Charity•Dikeh (@tontolet) on


A post shared by Tonto•Charity•Dikeh (@tontolet) on


0 Comments: