JINA la msanii wa Bongo Fleva Tunda Man katika muziki wa Bongo Fleva linajulikana kila mahali na hiyo inatokana na uwezo wake wa kutunga na kuimba mashairi ya muziki huo.
Uwezo wake umesababisha mashabiki wa muziki huo kumuunga na hiyo inatokana na kutambua kazi nzuri anayoifanya tangu alipoanza muziki.
Tunafahamu kuna wasanii wengi ambao waliimba na kupata umaarufu mkubwa na leo hii hawasikiki kabisa zaidi ya kubaki majina yao tu.Sio kwa Tunda Man maana licha ya kuwapo kwenye game kwa muda mrefu ameendelea kuonesha uwezo wake.
Ni msanii anayejua kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye muziki wa Bongo Fleva na kubwa zaidi anao uwezo wa kutambua apite njia ipi ili afike anakotaka kwenda.Ndio maana hajawahi kuyumba, siku zote anaendelea kufanya muziki wa kiwango cha hali ya juu.
Kwa sasa Tunda Man anatamba na wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la Shauri Yako ambaoo umerekodiwa kwenye studio ya T Touch.
Akizungumza kwenye moja ya mahojiano yake , Tunda Man anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu hivyo anatambua ukubwa wa jina lake na anataka aendelee kuwa bora kwa kutoa kazi nzuri.
Anasema kikubwa ambacho amekuwa akikifanya ni kuhakikisha nyimbo yake na video zinaendana na hiyo imefanya asiwepo shabiki wa kulalamikia ubora wa nyimbo au video ambazo anazitoa.
Kwa kukumbusha, Tund Man umaarufu wake umetokana na uwezo wake ambao amekuwa akiuonesha kwenye kundi lao la Tip Top Connecton. Kwa sasa kundi hilo licha ya kuwa bado lipo lakini ni kama vile limepoteza mwelekeo kwa kile kinachodaiwa kuwa anayelisimamia ameliweka kando na kujikita lebo ya WCB.
Akifafanua zaidi kuhusu kazi zake za muziki Tunda Man anasema yupo kwa muda mrefu kwenye muziki , hivyo lazima aoneshe kuwa yupo na hivyo mbali ya kuendelea kutoa nyimbo kali anayo studio yake.
Anasema studio hiyo ndio itakuwa inatumika kwa ajili ya kutengeneza muziki wake na wakati huo huo kuwasaidia wasanii wengine chipukuzi ambao wataonesha kuwa na uwezo wa kufanya muziki wa biashara maana siku hizi msanii si kuimba tu bali ajue muziki ni biashara.
“Muziki siku hizi ni biashara, lazima msanii anayetaka kufanya kazi na mimi ajue tunafakiwa kufanya muziki ambao utakuwa wa biashara.Hivyo hata wasanii ambao watakaotaka kufanya kazi kwenye studio yangu ninawashauri wafahamu muziki siku hizi ni biashara,”anasema Tunda Man.
Iwapo atakuwa na lebo kwa ajili ya kusimamia wasanii, Tiunda Man anasema yeye kwenye studio yake ataitumia zaidi kuwasaidia wasanii ambao wapo mtaani na wanao uwezo wa kuimba lakini wanakosa sapoti kidogo ya kuwafikisha wanakotaka.
Kuhusu baadhi ya nyimbo zake kuwashirikisha wasanii wasiokuwa na majina makubwa kwenye muziki anasema inatokana na kutambua kuwa unapomshirikisha msanii maarufu kuna wakati utakamkosa unapokuwa kwenye shoo, hivyo lazima uwe na msanii ambaye ukimhitaji inakuwa rahisi kupatikana.
“Wimbo mpya wa Shauri Yako nimeshirikisha msanii mchanga tu lakini anakipaji cha hali ya juu katika kuimba.Wakati naandaa huu wimbo nilitamani kumshirikisha msanii maarufu lakini baadae nikakumbuka
“Iwapo atakuwa na shoo sehemu halafu na mimi kuna sehemu natakiwa kuwepo itakuaje? Hivyo nimemshirikisha msanii ambaye ikitokea nahitaji kwenda kufanya kazi za muziki basi nikiwambia inakuwa rahisi kupatikana,”anasema Tunda Man.
Wakati akiendelea kufanya muziki wa kibiashara Tunda Man kwenye Mwezi wa Ramadhan uliomalizika hivi karibuni aliamua kutoa nyimbo za Kaswida kwa ajili ya mashabiki wake waliokuwa kwenye mfungo ambapo wakati anazungumzia kuhusu nyimbo za kaswada alisema kuwa iwapo atakuwa hai , basi hata mwakani atatunga nyimbo kwa ajili ya mwezi wa Ramadhan.

0 Comments:
Post a Comment