Bifu la Nicki Minaj na Remy Ma lilizidi kuwa kubwa baada ya Remy Ma kutwaa tuzo ya BET BEST FEMALE RAPPER lakini licha ya bifu lao kuwa kubwa Lil Kim alishasikika katika mahojiano na kituo cha Billboard kuhusu bifu hilo ambapo amesema hana mpango wa kuungana na Remy Ma kumdiss Nicki Minaj.
Lil Kim ambaye alishamdiss NickiMinaj kupitia ngoma ya ‘Black Friday’ aliongeza hana bifu kabisa na Nicki kwa kuwa walishamaliza na kikubwa anachoweza kueleza kuhusu marapa hao wa kike ni kuwashirikisha wote wawili katika album yake mpya.








0 Comments:
Post a Comment