Wednesday, July 19, 2017

Tonto Dikeh aokoka, azaliwa upya

MSANII nyota wa Nollywood, Tonto Dikeh ameamua kumrudia Mungu na kutubu baada ya kutukanana na mama mkwe wake wa zamani.
Tukio hilo la kutukanana lilitokea wiki chache zilizopita, hivyo aliamua kutumia mitandao yake ya kijamii kujutia kitendo hicho.
Mwanadada huyo mwenye mtoto mmoja, amejivunia kurudi katika mikono salama ya Yesu na anaamini yupo katika njia sahihi.
Katika mtandao wake wa Kijamii wa Instagram aliandika:” Ninajivunia kuzaliwa tena mkristo, ukristo ndio dini yangu na ndio maisha yangu.
“Nimeruhusu nguvu za Mungu zije kwangu, hakuna silaha itakayotengenezwa kunidhuru au kumdhuru mwanangu au wafanyakazi wangu kwani namuamini Yesu...Amen.

0 Comments: