Friday, July 28, 2017

Stephanie ajivunia kuolewa mapema

MWANADADA anayefanya vizuri katika filamu za Kinigeria, Stephanie Okereke-Linus, amesema tangu aolewe amekuwa mwanamke mwenye furaha duniani.
Ujasiri huo ameupata baada ya mwanadada huyo kuwa mbali na vyombo vya habari, kitu ambacho kimemfanya aendelee kuheshimika katika jamii yake.
Alisema amepata uzoefu mkubwa katika maisha ya ndoa anayoishi hivi sasa kwakuwa aliyeamua kuolewa naye anampenda na kumjali.
“Hakuna ninachojutia kwa sasa kwakuwa nimeolewa, ninamuamini Mungu kwani ndiye mpanga wa yote, nafurahia maisha yangu kwa sasa,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu kupata mtoto, alisema hayo ni masuala binafsi kati yangu na muwe wangu na kwamba hatuwezi kuweka kila kitu wazi kwa kila mmoja.

0 Comments: