Friday, July 28, 2017

Familia yataka Ali Kiba afunge ndoa

FAMILIA ya Mfalme wa Bongo Fleva Ali Kiba imesema ni wakati muafaka kwa kijana wao kupata jiko hasa kwa kuzingatia umri alionao unaruhus.
Kauli hiyo inakuja wakati Ali Kiba akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo namba katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006 Jokate Mwegelo.
Hivyo familia hiyo imesema ni wakati muafaka kwa Ali kufunga ndoa ili apate mke atakayelea watoto wake wanne ambaye kila mmoja ana mama yake.
“Kama ujana ameshafanya sana Ali na sasa ni wakati muafaka wa yeye kuoa ili awe na mke.Hakuna ambacho hajakifanya katika umri alionao na ndio maana tunaona huu ni muda sahihi wa kuoa,”anasema mmoja ya wanafamilia.

0 Comments: