Wednesday, July 19, 2017

Ramsey, Omoni waleta gumzo mtaani

WASANII wa filamu za Nollywood, Ramsey Noah na Omoni Oboli, wamezua mjadala kutokana na mavazi waliyovaa katika fimu mpya ya ‘Mke wangu na mimi’.
Filamu hiyo inayoelezwa kuwa ni ya vichekesho imeongozwa na Chinaza Onuzo ambapo katika picha walizoweka katika mitandao ya kijamii walionekana wamevaa nguo kuu kuu.
Wasanii hao watacheza katika filamu hiyo wakiwa na majukumu tofauti.
Filamu hiyo inaelezea changamoto za wana ndoa wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku na jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Wasanii wengine waliopo katika filamu hiyo ni Ngozi Nwosu, Sambasa Nzeribe, Jemima Osunde na Rachael Oniga.
Filamu hiyo inaaminika itakuwa nzuri itakayokufanya uchangamke na kupoza uchovu uliokuwa nao.

0 Comments: