Unapozungumzia mastaa wa kike ambao wameonesha kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja kwa muda mrefu basi ni pamoja na Naj ambaye kimsingi anaonekana kuwa hayumbishwi na hisia za mapenzi, hali ambayo inamfanya yeye na Baraka The Prince kuendelea kufurahia uhusiano wao.
Siku za karibuni, Baraka The Prince hakusita kumuelezea Naji na hasa uhusiano wao ambao umekuwa ukiimarika kila siku huku akitumia nafasi yake kumwagia sifa kibao na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ili umma ujue.

“Kwanza naomba ieleweke Naj ni mchumba wangu na si mke, tunafahamu mke ni hatua kubwa zaidi kwenye mahusiano ya kimapenzi ila sisi tupo kwenye hatua ya uchumba.Hivyo Naj ni mchumba wangu,”anasema.
Pia uhusiano wao umewafanya wawili hao kutumia muda wao mwingi kuwasiliana iwapo mmoja atakuwa mbali na mwenzie na ndio maana kwa siku wanachat mara nyingi zaidi kwani haiwezi kupita dakika tatu bila kuwasiliana kwenye simu.

Pamoja na yote Baraka The Prince anasema anamwamini sana Naj, hivyo hata ikitokea siku akapata tetesi kuwa ana mtu mwingine itakuwa ngumu kwake kuamini kwani haiwezekani.







0 Comments:
Post a Comment