Saturday, July 15, 2017

Mlela aelezea alivyonusurika kifo Kenya

MBONGO Muvi  Yusuf Mlela ameeleza namna ambavyo amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya  gari na kusababisha alazwe hospitali ili kutetea uhai wake.

Mlela alipata ajali akiwa nchini Kenya, wakati anaelekea  klabu kuhudhuria shoo ya wasanii kutoka Bongo, Ben Pol na G-Nako.Alikuwa akitumia gari akiwa na rafiki zake , lakini ghafla walipoteza muelekeo na kwenda kugonga kalavati ambapo yeye alipoteza fahamu na kuchanika mdomo kwa juu.

“Mwendo ulikuwa wa kawaida lakini cha kushangaza tukiwa njiani gari ikaanza kuyumba, hali iliyosababisha dereva kushindwa kulidhibiti.Tukagonga kalavati na baada ya hapo nilikuja kupata fahamu nikiwa hospitalini,”anasema na kuongeza anamshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa uhai.

0 Comments: