Saturday, July 15, 2017

Rihanna kushiriki maonesho ya mavazi


MWANAMUZIKI  Rihanna anatarajia kuwa miongoni mwa watakaoshiriki kwenye onesho la mavazi  New York Fashion Week -Marekani, akiwa na bidhaa yake ya Fenty Puma aliyoizindua mwaka juzi.

Taarifa iliyopo mtandaoni inaeleza kuwa katika onesho hilo Rihanna anatarajiwa kuonesha mavazi yatakayotumika kipindi cha mwaka 2018.
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa msanii huyo kuonesha mavazi yake katika wiki ya mitindo tangu alipozindua mwaka 2016 kabla ya kuzipeleka Paris Fashion Week kuzindua msimu wa mavazi hayo kwa mwaka 2017.

0 Comments: