Saturday, July 22, 2017

‘Bado sijajifungua , nitawaambia mwenyewe’


MSANII  Linah Sanga   amewaomba mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kupuuza habari zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejifungua kwani hazina ukweli wowote na wakati ukifika atawaambia yeye mwenyewe.
Linah amesema anashangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni na hajui ni nani ambaye anazisambaza na malengo yake ni yapi.
“Sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyesambaza taarifa hizo ana malengo gani? Nawaomba mashabiki zangu waniombee kwani nakaribia kwenda kujifungua ingawa siwezi kusema ni lini maana si vizuri,”anasema.

0 Comments: