Tuesday, July 25, 2017

Ebitoke yaani 'kafa ...kaoza' kwa Ben Pol


'KISI ni noma'Hiyo ndio unaweza kuilelezea kwa mwanadada ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya kuigiza vichekesho Ebitoke ambaye kwa sasa amenasa kwenye penzi jipya la Ben Pol.

Kilio cha Ebitoke kilipata nafasi ya kusikika baada ya Ben Po kuamua kujiweka rasmi na kinachoendelea sasa ni kuponda raha baada ya kutumia muda mwingi akitumia mitandano ya kijamii akielezea namna ambavyo anatamani awe mumewe.

Hata hivyo cha kufurahisha zaidi ni pale Ebitoke anapoamua kuweka hadharani kuwa anakumbuka siku ya kwanza ambayo amepata kissi kutoka kwa Ben Pol kwani anahisi alikuwa kwenye ulimwengu tofauti na huu ambao tumeuzoea.

"Kisi la Ben Pol likanifanya nihisi nipo mbinguni,ni kisi ambalo limeweka historia katika ukurasa mpya wa mapenzi hasa kwa kuzingatia ndio mwanaume wangu wa kwanza,"anasema Ebitoke.

Anasisitiza anampenda Ben Pol na anafurahia uwepo wake na ndio maana alipopata kisi alijiona kama vile mwili umepata baridi ambayo hajawahi kuisikia.

"Hakuna jambo nzuri kama inapotokea mtu unayempenda halafu akatokea akakukiss lazima mwili usisimke."

0 Comments: