Saturday, July 22, 2017

Flora Mbasha avunja ukimya

MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injil Flora Mbasha amevunja ukimya na kusema anachukizwa na watu ambao wanatumia mitandao ya kijamii kumchafua.
Flora ametoa kauli hiyo juzi baada ya kusambaa taarifa mitandaoni akinukuliwa mzazi mwenziye akisema hakuwahi kumridhisha kimapenzi kwa kipindi chote walichokuwa kwenye ndoa.
Flora amekana taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika hivi: “Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na redio yoyote na kuzungumza maneno hayo kama ilivyosambaa mitandaoni.
“Naomba mzipuuze taarifa hizo maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonesha upuuzi wake ili apate followers kwenye ukurasa wake.Hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia stori za uongo asifikiri siijui sheria, ajipange vizuri maana mahakama ipo na sheria ipo”anasema.

0 Comments: