Saturday, July 1, 2017

Audu: Mume wangu hunifundisha ‘kukiss’

MSANII wa kike wa Nollywood, Esther Audu ambaye ameolewa na Phillip Ojire, ameweka wazi jinsi alivyopambana kuishi maisha ya ndoa huku akiendelea na kazi yake ya usanii.
Audu alisema mumewe amekuwa akimsapoti kwa kiasi kikubwa hasa akimtia moyo katika sehemu anazocheza na kumbusu msanii mwenzake.
Akizungumza na mjini hapa,  Audu alisema ni kweli ameolewa lakini hakuna kitu kilichobadilika kwake na kwamba amebaki kama Esther uliyemfahamu.
Alisema kitu cha tofauti kwa sasa ni kwamba amekuwa mke wa Ojire lakini kwa upande mwingine anaishi maisha yake ya kawaida.
“Kitu cha bahati kwangu ni kwamba mume wangu ananisapoti katika uigizaji. Pia ni mtu wa burudani, ni muongozi wa nyimbo katika utengenezaji wa video, hivyo anaelewa ni aina gani ya kazi ninayoifanya.î alisema.

0 Comments: