Sunday, June 25, 2017

Zari aacha ofisi ili atetee penzi lake kwa Diamond

ZARI ‘The Boss Lady’ ameamua kuacha ofisi ili aweze kutetea penzi lake kwa Diamond! Hiyo ndio habari ya mjini kwa sasa baada siku za karibuni Nasseb Abdul ‘Diamond Platnum’ kuposti maelezo ya kuonesha hana imani na Zarina Hassan a.k.a Zari  baada ya kuona picha akiwa anaogolea na mwanaume mwingine.
Picha hiyo ilimfanya Diamond kuweka ujumbe ambao uliashiria kuwa penzi lao limetikiswa na kwa kutumia akaunti yake ya mtandaoni alitoa maneno makali dhidi ya Zari.Hata hivyo baadae aliamua kuyatoa na hadi sasa hakuna alichoweka tena ila juzi sasa amefunguka na kueleza kwa kifupi kilichotokea.
Diamond anasema “Baada ya post yangu ya insta wasanii wengi walinipigia simu, Psquare na Fally Ipupa walinicheki kutaka kujua nini kimenikuta,” alisema Diamond.
Anasema baada ya kupost picha na ujumbe ambao haukuwa mzuri kwa Zari, mrembo huyo wa bosi wa WCB alionyesha kutofurahishwa na ujumbe huo.
“Baada ya Zari kuona post yangu Insta alikuwa ofisini na alirudi nyumbani na aliponielewesha nilikuwa mpole na nikamuelewa.Sikuwa na cha kusema tena imebidi niwe mpole
“Nahisi nilikurupuka ila kumbuka na mimi ni binadamu, hivyo wivu upo na nilipoona vile sikuweza kuvumilia ndio maana nikaposti ule ujumbe.Baada ya kunielewesha nimemuelewa,”anafafanua Diamond.

0 Comments: