Saturday, June 24, 2017

Nyumba ya wazazi ya Madonna yaingizwa sokoni

NYUMBA ambayo alikuwa anaishi malkia wa muziki wa pop duniani Madonna katika kipindi cha utoto wake akiwa na wazazi wake imeingizwa sokoni.
Mwaka 2008 nyumba hiyo iliyopo Mji wa Detroit, Michigan nchini Marekani, iliungua kwa moto na iliachwa wazi mpaka kufikia mwaka 2012 ndipo ilipouzwa kwa Sh 205,041,035.
Hivyo kwa sasa nyumba hiyo yenye vyumba vitano vya kulala, mabafu matatu ilitengenezwa vizuri na mwenye nyumba huyo mpya inauzwa kwa Sh 1,073,226,252.

0 Comments: