Sunday, June 25, 2017

Amber Lulu awaumbua mastaa wa kiume


MREMBO kwenye  muziki wa kizazi kipya  Amber Lulu amesema mastaa wengi katika kiwanda cha burudani ni wasumbufu hasa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Akipa stori katikati ya wiki hii Amber anasisitiza Mastaa wengi bongo ni wasumbufu sana, na yeye huko nyuma aliwahi kuwa katika mahusianio na hao mastaa akaona bora aachane nao.
“Naona  walivyo kwa sasa na najua wanavyoishi ndio mana sina mpango nao.Mastaa wengi hawako serious na hata kwenye maisha yao hawako serious, mie naona mastaa naoshindanao,”anasema Amber.
Amefafanua akili yake kwa sasa ni kujiimarisha zaidi katika kufanya muziki wake kuliko kuendelea kuonekana tu kwenye video za wasanii wengine.

0 Comments: