Saturday, June 10, 2017

Riyama amzungumzia ndoa yake

MWIGIZAJI wa filamu Riyama Ally na mumewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Leo Mysterio wameweka wazi kuwa hakuna tatizo la wao kuona aibu kuishi pamoja, eti kwasababu wametofautiana miaka saba.
Akipiga stori wiki hii, Riyama Ally anasema binafsi haoni aibu wala hana hofu kuolewa na mwanaume ambaye yeye amemzidi umri zaidi ya miaka saba, wakati Mysterio anasema  alipokuwa anajiandaa kumuoa Riyama anakiri  alisemwa na kukosolewa.
“Tumependana na ndio maana leo tunaishi mume na mke, umri si tatizo kwetu na ndio maana tumefunga  ndoa. Sisi ni watu wa dini lazima mambo yaende kwa mujibu wa dini inavyotaka.
“Niliwahi kutoa  kibao maaalumu cha wimbo kuhusu Riyama na nilitunga kutoka mashairi na kuyaimba kutoka moyoni na nakumbuka niliwashangaza wengi,”anasema Mysterio.

0 Comments: