Saturday, June 24, 2017

Penzi la Jenner, Scott lashika kasi

MAHABA niue! Ndivyo unaweza kusema kwa staa Kylie Jenner na rapper Travis Scott ambapo kwa sasa wameendelea kuonesha mahusiano yao yanavyozidi kuimarika kila kukicha.
Katika kuthibitisha mambo yao yapo vizuri wawili hao wameamua kuchora tattoo zinazofanana katika miguu yao.
Juzi kati mtandao wa Snapchat, Jenner ameweka picha inayoonyesha akiwa amechora totoo ya kipepeo chini ya mguu wake wa kulia na Scott akiwa amechora tattoo kama hiyo sehemu ya chini ya mguu wake wa kushoto.

0 Comments: