Saturday, June 24, 2017

Mamisa afurahia Young D kukubali kulea mtoto

HATIMAYE mzazi mwenza wa mkali wa Singo ya Bongo bahati mbaya, David Genzi a.k.a Young D’,  Mamisa amefunguka na kueleza amemaliza tofauti zake na jamaa huyo baada ya kukubali kumlea mwanaye ambaye mwnzoni alidaiwa kuwa amemtelekeza.
Akizungumza wiki hii Mamisa anasema wameamua kumaliza tofauti zao wao wenyewe bila kumshirikisha mtu na Young D amekubali kuwa baba bora kwa mwanaye.
“Mungu amenisimamia na kwa sasa nipo sawa na mzazi mwenzangu, tuliyaongea bila kuwekwa kikao na mtu yeyote. Young D amem-chukua mtoto na anaishi na bibi yake (mama wa Young D),”anasema Mamisa.

0 Comments: