Saturday, June 24, 2017

Nay aipua mpya, arusha kijembe

RAPA Nay wa Mitego Alhamisi ya wiki hii ameaachia wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la  Moto  ambayo amwewaunguza baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo flava.
Wimbo huo unakuja siku moja tu baada ya Diamond kuachia ngoma yake mpya ‘Fire’ aliyomshirikisha Tiwa Savage kutoka Nigeria ambayo inazungumzia mapenzi.Kwa upande wa Nay ameamua kuwachana baadhi ya watu wakiwemo wasanii na mameneja wa muziki hapa nchini.
Kwa kutumia mtandao wake wa Instagram, Nay amewataja pia wasanii ambao wanaamini wao wakiondoka katika game ya muziki basi mapengo yao hayawezi kuzibika.
“Eti Pengo Lako alizibiki.?! Siku izi Mapengo yanazibika tu.! Pengo la @kingzilla_tz ni @billnass Nafasi ya @iamrubyafrica Ni @officialnandy,” ameandika Nay kwenye mtandao huo.

0 Comments: