Saturday, June 24, 2017

Obi Ogodo: Wasanii hujipeleka wenyewe kwa wanasiasa

MSANII anayekuja kwa kasia katika tasnia ya filamu za Nollywood, Sapphire Obi Ogodo, ameweka wazi jinsi wasanii wenzake wa kike wasivyo waaminifu kwa wapenzi au waume zao.
Kwa mujibu wa mwanadada huyo ambaye aliyazungumza hayo wakati akizungumzia filamu aliyocheza akijiuza kanisani, wanawake wengi maarufu hutumia umaarufu wao kufanya mapenzi na wanasiasa.
“Wengi wao ambao ni maarufu hawataki ndoa, ila hupenda kujaribu na kuona kama jamii itawakubali. Wakati wakiwa na wapenzi wao, huwa na mwanaume mwingine katika sehemu tofauti,” alisema na kuongeza;
“Utakuwa lazima awe na mtu mkubwa au mwanasiasa yeyote. Baada ya kutoka na watu wenye majina, hurudi nyumbani na kuwaambia waume zao kitu kimoja, hajisikii kufanya mapenzi kwakuwa alikuwa na shughuli kubwa alipotoka. Tunatakiwa kuangalia upya matendo yetu.

0 Comments: