Saturday, June 24, 2017

Mpenzi wa Iyanya apiga picha za utupu

MPENZI wa zamani wa mwanamuziki, Iyanya, Yvonne Nelson, amewaacha mdomo wazi mashabiki wake kwa kuweka picha zake akiwa nusu uchi.
Mwanadada huyo ambaye ni mbunifu na mwanamitindo maarufu, aliweka picha yake kipande katika mtandao wake wa kijamii akiwa hana nguo.
Yvonne ambaye ni miongoni mwa wanyange waliofanya vizuri katika tasnia hiyo barani Afrika, ameacha gumzo kutokana na picha hiyo.
Lakini wabobezi wa masuala ya kijamii, wanaeleza kwamba kwa kufanya hivyo ameshusha utu wake kitu ambacho kitakuwa kikizungumzwa kila kukicha.


0 Comments: