Saturday, June 24, 2017

Mercy Aigbe awa Balozi wa Wajane

NYOTA anayefanya vizuri Nollywood, Mercy Aigbe ameteuliwa kuwa Balozi wa Mfuko wa Wajane wa Liberty.
Uteuzi huo umefanywa na Mratibu wa maadhimisho ya siku ya kilele cha Wajane, Felix King ambaye alithibitisha kumteua mwanadada huyo kuwa balozi wao.
Mwanadada huyo mwishoni mwa wiki, aliwaambia mashabiki wake juu ya nia ya ke ya kuwa balozi wa mfuko na atashiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika Mji wa Benini.
Alisema amepata sapoti kubwa kutoka kila kona ya dunia juu ya uamuzi huo na kwamba atapambana kupinga vitendo vyovyote vibaya wanavyofanyiwa wajane.
Aliongeza anaomba jamii uingane kwa pamoja kupinga vitendo hivyo vitakavyosababisha kuleta mgawanyiko ndani yake.

0 Comments: