Saturday, June 24, 2017

Dogo Janja amkana Muna Love

MSANII  wa  muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema hana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji  wa zamani Muna Love.
Amesisitiza hajawahi kuwa na uhusiano na mwanadada huyo ambaye pia ni mfanyabishara na habari hizo zimemuweka sehemu mbaya kwenye uhusiano wake na mpenzi wake na kwenye familia yake pia.
Amelazimika kueleza hayo baada ya tetesi kuenea muda mrefu kujihusisha na mwanadada huyo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kudai Dogo mbali ya mapenzi amefuata mteremko wa maisha kwani analelewa na Muna Love.
“Niseme tu kama kuna kitu kibaya basi ni huu utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka asubuhi anajisikia kufanya chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini si kitu kizuri,
“Maana yananiumiza mimi na familia yangu, uongozi wangu lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa,hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya”, Dogo Janja alifunguka.
Anasema yeye si msanii wa kuonesha maisha yake binafsi kwenye mitandao ndio maana hata mpenzi wake hajwahi  kumuweka mitandaoni.

0 Comments: