Saturday, June 10, 2017

Mtoto wa Wizkid ateguka shingo ajalini


MTOTO wa pili wa mwanamuziki nyota nchini Nigeria, Wizkid ambaye ni King Ayo, amekimbizwa hospitalini baada ya kuteguka shingo katika ajali nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo, Binta Diallo, mtoto wake amekimbizwa hospitali baada ya kutokea kwa ajali hiyo ya kutisha.
Baada ya kupatiwa matibabu, aliweka picha ya mtoto huyo katika mitandano ya kijamii akiwa amefungwa bandeji katika shingo yake.
Picha hiyo ilikuwa na maelezo:” Sikuwa katika hali ya kawaida wakati mtoto wangu wa kiume alivyopata ajali, niliumia sana kushuhudia tukio la kusikitisha.
“Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwanini imetokea hivi ila Mungu pekee ndiye anayejua sababu yake, namuomba Mungu aendelee kumlinda mwanangu,”.


0 Comments: