Saturday, June 10, 2017

Wamekutana ndani ya ngoma ‘tatu chafu’


BILA kupoteza muda leo ningependa kukumbusha mastaa wa muziki wa Bongo Fleva waliokutana kwenye kolabo tatu zenye uzito usiopimika hata kwa mizani.
Katika ngoma hizi tatu zinaweza kuwa wameshirikishwa na msanii mwingine au wao kwa wao, ila hii haiwahusu wale walio katika kundi moja au lebo, twende tukawatazame.

Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz
Kila mmoja ana heshima yake katika muziki wa Bongo Fleva, na kila mmoja ana ngome yake anayoiwakilisha.
Diamond akiwakilisha WCB Wasafi na Ommy Dimpoz akiwakilisha Pozi kwa Pozi (PKP), hizi zote kwa sasa ni lebo za muziki zinazosimamia wasanii, tuachane na hilo.
Wawili hawa kwa mara ya kwanza walikutana kwenye wimbo wa Dully Sykes iliyokwenda kwa jina la ëUtamuí, kazi hii iliwakutanisha watu wenye ujuzi wa kucheza na sauti zao na ndio sababu hata wimbo huu ulifanya vizuri.

Haikuishia hapo, wakaja kukutana tena kwenye remix ya wimbo wa ‘Piga simu’ wa mtangazaji wa Clouds fm, Diva, kwa mara ya kwanza Diva aliufanya wimbo huu na Diamond pekee yake.
Safari yao ya mwisho katika kolabo ni pale walipopewa shavu na Victoria Kimani kutoka Kenya kwenye wimbo wake wa ‘Prokoto’, wimbo huu ulifanya vizuri sana kimataifa na ulifungua milango kwa wasanii hawa kuzidi kutambulika nje.
Chukua na hii, Diamond na Ommy Dimpoz hawajawahi kuwa na wimbo wao wa pamoja.

Mr Bule, Lady Jaydee
Kabla ya yote ningependa utambue kwamba Mr Blue ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva aliyofanya kolabo nyingi sana akitanguliwa na Chid Benz.
Wimbo wa kwanza kukutana ulikuwa unaitwa ‘Wapambe’ ambao ni wa Mr Blue, ni wimbo wa kitambo kidogo na ni mashabiki wacheche wa Bongo Fleva wanaoujua.
Mr Blue hakuishia hapo, akampa tena shavu Lady Jaydee kwenye wimbo unaofahamika kama ‘Sema’, lakini nyimbo zote hizi mbili Lady Jaydee ameshiriki kwa kiasi kidogo.
Kolabo yao ya tatu inakamilika baada ya Lady Jaydee kumpa shavu Mr Blue kwenye wimbo wake wa ëWanguí ambao ulifanya vizuri kuliko nyimbo za awali walizofanya pamoja.

AY,Fid Q
Hapa unakutana muziki wa hip hop ‘commercial’ na hip hop ‘hardcore’, AY akiwakilisha Green City Mbeya, huku Fid Q akiwakilisha Rock City Mwanza.
 Kwa mara ya kwanza wanakutana kwenye wimbo unaofahamika kama ëUjio wa Vesi Mojaí ambao ni wa Fid Q, kama unakumbua baadhi ya mistari wimbo huo Fid Q kairudia kwenye wimbo wa Agosti 13.

Siku hazigandi, wanakutana tena kwenye wimbo uitwao ëShimo Limetemaí ambao ni wa Fid Q, katika wimbo huu ameshirikishwa Reuben Ndege ëNcha Kalií aliyekuwa mtangazaji wa redio kwa kipindi cha nyuma.
Mwishoni AY na Fid Q wanaamua kutoa wimbo wa pamoja uliofahamika kama ‘Jipe Shavu’ wakieleza ëmitikasií ya kupata fedha.
Chukua na hii tena, sauti ya Fid q ndio husikika mwishoni mwa ngoma ya AY ‘Mikono Juu’. Maneno aliyozungumza katika wimbo huo inasemakana yalikuwa yanamlenga rapa Rado ambaye walikuwa hawaelewani.

Jux,G Nako
Kwa kipindi cha hivi karibuni Jux amekuwa karibu sana na kundi la Weusi na wameshafanya kazi nyingi pamoja.
Wimbo wa kwanza kufanya ni ‘Safari’ ambao walishirikishwa na Nikk wa Pili, bila shaka utakuwa unaukumbuka na nilishawahi kuuchambua kwenye safu hii.
Kwa mara ya pili wanakutana kwenye wimbo wa Quick Rocka unaojulikana kama ‘Hapo’ ambao ulitoka katikati ya mwaka huu na kufanya vizuri kwa kiasi fulani.

Safari ya kuelekea kwenye ngoma zao ëtatu chafuí inagota kwenye remix ya wimbo wa ‘Movie burger selfie’ wa Belle 9 ambao ndani yake kuna Izzo Business, Maua Sama na Mr Blue.
Mwaka huu wamekutana katika wimbo wao pamoja ambao unakuwa wa nne. Wimbo unaitwa Go Low ambao umetengenezwa na prodyuza Luffa.
Peter Akaro
Kwa maoni 0755 299 596

0 Comments: