Saturday, June 24, 2017

Doyle aeleza alivyopata ujauzito akiwa mtoto

MSANII mkongwe wa Nollywood, Iretiola Doyle, ameeleza jinsi familia ilivyoshindwa kumuamini baada ya kupata ujauzito akiwa na miaka 17.
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akitoa ushuhuda katika Kituo cha Dini ya Kikristo cha Harvesters jijini Lagos.
“Umezungukwa na watu wanaokupenda na kukusapoti. Nilibarikiwa kuzungukwa na watu hao, lakini kwa bahati mbaya hawakuwa familia yangu.Mama yangu hakuichukulia kwa wepesi.
“Nililazimika kuendana na hali hiyo kwakuwa nilitoka katika kizazi kingine. Niliumizwa na watu niliokutana nao na walinieleza siwezi kuwa na maisha mabaya kwa hali niliyokuwa nayo.
“Kuzungumza na vijana wadogo ni kitu kizuri, ukiniuliza waziri wako ni nani nitakujibu ni kuwafikia vijana wa kike,” alisema.
Aliongeza ikitokea katika maisha kuna mtu anakuelekeza ulipokosea, ni lazima utambue uhusiano wako na huyo mtu hata kama si ndugu yako.

0 Comments: