Sunday, June 25, 2017

Gigy Money awatolea uvivu warembo

STAA Gigy Money ameamua kuweka wazi kuwa si lazima kwa warembo wanaofanya kazi kama yake waingie kwenye muziki wa kizazi kipya.
Akizungumza siku za karibuni Gigy Money ameeleza kuingia katika muziki kuna baadhi ya watu wanachukulia poa lakini watambue yupo makini na muziki.
“Najua si lazima wote tuwe waimbaji  lakini kibongo bongo ukifanya vile sana unakuwa huwezi kufanya na mambo mengine, yaani hutoboi. Watu wanakuona wewe miyeyusho,
“Yaani wewe huna akili kwa sababu watu wanachukulia Gigy ni mtu kalanduka, kapinda kumbe mimi niliangalia hela, halafu niliangalia na mkwanja,”anasema.
Anaongeza kuwa yupo ‘serious’ na kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kutoa video ya wimbo wake mpya baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhan.”Najiandaa kufanya balaa kwenye muziki maana nakuja na kibao kinaitwa Papa”.

0 Comments: