Sunday, June 25, 2017

Jokate aeleza anachotamani kwenye maisha yake

MREMBO  Jokate Mwegelo, maarufu kwa jina la Kidoti ameeleza kitu ambacho anatamani kukiona kikitokea kwenye maisha yake mbali ya maisha mazuri kubwa ni kupata watoto mapacha.
Akizungumza wiki hii jijini Dar es Salaam Jokate ambaye mbali ya kuwa mrembo amekuwa mjasiriamali na mwanamitindo anasema anapenda sana kuwa na watoto mapacha.Nani anatakayezaa naye anasema siku si nyingi atamuweka hadharani mume wake.
“Napenda nipate watoto mapacha na wote niwalee maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote,” Jokate.

0 Comments: