Saturday, May 20, 2017

Wasanii waungana kupinga unyanyasaji wanawake, watoto

Mercy Johnson-Okojie
WASANII nyota wa filamu nchini hapa (Nollywood), wameunga mkono kampeni maalumu iliyowekwa na Serikali kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto.
Mratibu wa muunganiko huo wa nyota hao, Uche Ogbodo, ambaye amekuwa mstari wa mbele kusapoti kampeni hiyo, anasema tayari nyota kama Mercy Johnson-Okojie, Chioma Akpotha, Uche Jombo, Omoni Oboli, Stephanie Linus, Annie Idibia ni baadhi ya wasanii ambao wameonesha sapoti ya wazi.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, kampeni hiyo itatoa thamani halisi ya wanawake na watoto. “Kupitia kampeni hii tunaimani tutawaelewesha Waafrika kwamba wanawake na watoto wanapaswa kuhudumiwa kwa uangalifu na upendo,” alisema Ogbodo.
Wasanii wengine ambao watajiunga katika kampeni hiyo ni pamoja na Halima Abubakar, Omotola, Yvonne Okoro, Kate Henshaw na Lilian Esoro.

0 Comments: